Umesahau Nywila?
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni miongoni mwa Taasisi za usimamizi wa masuala ya Utawala Bora nchini Tanzania iliyoundwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (Sura ya Pili ya Sheria za nchi). Jukumu la msingi la Sekretarieti ni Kukuza na Kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma, kwa kuzingatia Dira ya Taasisi ambayo ni kuwa kitovu cha bora na ufanisi katika kukuza na kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma. Kupokea a kuhakiki taarifa za Rasilimali na madeni ya Viongozi wa Umma ni moja ya jukumu la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lililoainishwa katika Sheria ya Maadili Na. 13 ya Mwaka 1995. Sheria inamtaka Kiongozi wa Umma kuwasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili kabla au ifikapo tarehe 31 Desemba kila Mwaka. Tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Maadili, Matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi yamekuwa yakipokelewa na kuwasilishwa Sekretarieti kwa nakala ngumu zoezi ambalo limekuwa na changamoto nyingi ikiwemo:- Gharama kubwa za uchapishaji wa fomu za Tamko na muda mwingi unaotumika kutuma fomu ili ziweze kuwafikia Viongozi. Ili kukabiliana na changamoto hizi Sekretarieti imeamua kuwekeza katika matumizi ya TEHAMA kwa kuanzisha Mfumo wa Ujazaji Matamko kwa njia ya Mandao (Online Declaration System -ODS). Kuhama kwenda katika matumizi ya TEHAMA kutaisaidia Sekretarieti kupunguza gharama hasa zile za uchapishaji wa fomu, usambazaji na wakati mwingine kuandika barua za kukiri kupokeaTamko. Mfumo wa ujazaji Matamko kwa njia ya Mandao (ODS) ni Mfumo mpya unaomuwezesha Kiongozi wa Umma kujaza Tamko la Rasilimali na Madeni na kuliwasilisha kwa Kamishna wa Maadili kwa nia ya Mandao. Mfumo huu utamuwezesha Kiongozi kutuma tamko lake akiwa sehemu yoyote na wakati wowote na zaidi utampunguzia gharama na muda aliokuwa akitumia kuwasilisha Tamko lake hapo awali. Ili kuweza kutumia mfumo huu Kiongozi atatakiwa kuwa na kompyuta na huduma ya intaneti. Ni matumaini yang kuwa kupitia mfumo huu hapatakuwa na Kiongozi atakaechelewa kuwasilisha Tamko au kushindwa kuwasilisha tamko.